mambo@oky.co.tz

Kutunza taarifa zako ni jambo la muhimu kwetu. Tunalenga kuwa na viwango vya juu vya faragha na ulinzi na tumejitolea kuwa wawazi juu ya jinsi tunavyochambua na kutumia taarifa zako. Hii sera faragha inaelezea kwajinsi gani taarifa zako zinakusanywa, kuhifadhiwa na kutumika, na ni hatua gani tunachukua kuhakikisha taarifa zako zinakuwa salama.

Tafadhali soma sera faragha yetu kwa umakini kabla hujatumia Oky na ipitie mara kwa mara kuona maboresho. Kumbuka, kwa kupata na kutumia app au tovuti ya Oky, umekubaliana na sera faragha hii.

Oky imetengenezwa na UNICEF. Tafadhali usisite kuwasiliana nasi kama una maswali yoyote juu ya kutumia taarifa ndani ya Oky. Kuwasiliana nasi tutumie barua pepe mambo@oky.co.tz .

Kwa dhumuni la sera faragha, “taarifa binafsi” inamaanisha taarifa yoyote inayotuwezesha kumtambua mtu, moja kwa moja au siyo moja kwa moja, kwakuangalia vitambuzi kama jina, namba ya kitambulisho,taarifa za eneo, vitambuzi vya kwenye mtandao au moja au sababu zaidi maalumu kwa mtu binafsi.

1.Je ni data zipi oky anzikusanya na jinsi zinavyotumika?

Unapoingiza taarifa ndani ya app ya Oky, Oky inatumia teknolojia kubadili ‘taarifa’ kuwa taarifa zenye manufaa ambazo zinaweza kukusaidia kujifunza zaidi juu ya mfumo wa mzunguko wako wa hedhi, kukusaidia wewe kuwa dereva wa mwili wako na afya yako.

Oky imetengenezwa kutumia kidogo taarifa zako binafsi. Zinazoelezewa hapo chini ni vyanzo na aina ya taarifa tunazokusanya na kuchambua pia taarifa ya jinsi tunavyotumia data hizi .

Ili kutumia kipengele cha kifuatiliaji cha hedhi kwenye app, lazima utengeneze kuingia. unapotengeneza kuingia, tunakuuliza juu ya kuonyesha au jina la mtumiaji, tarehe yakuzaliwa, jinsia na eneo. Tunakuhamasisha uchague jina ambalo halifanani jina lako halisi au taarifa nyingine ambazo zinaweza kukutambulisha – sana sana kama una umri chini ya miaka 18. Tunaomba hivi; jinsia, umri na taarifa ya eneo kutoka kwako ili kuelewa kama tunafikia wahusika sahihi. Taarifa zote hizi hukusanywa kwa pamoja na kufichwa utambulisho

Taarifa za kifaa



Tunakusanya taarifa kwenye kifaa utumiacho kupata huduma za Oky ’ kama modeli, mfumo wa uendeshaji, lugha, eneo na muda wa kipindi. Taarifa hii haina utambulisho na inakusanywa kutusaidia kuwaelewa watumiaji wetu vizuri na jinsi wanavyoshiriki kwenye Oky.
Taarifa za ushiriki/utumiaji.

Unapotumia app ya Oky, sisi na watoa huduma wa nje tunachukua taarifa jinsi unavyotumia app ya oky. Taarifa za utumiaji haina utambulisho wako binafsi. Tunatumia kituo cha app pamoja na vipengele vilivyotengenezwa kufuatilia ili kurekodi matumizi haya.

Tukusanya taarifa hizi ili kuelewa matumizi yako kwenye huduma yetu, kwa mfano ni kazi zipi kwenye app unatumia na kuhakikisha vipengele vitolewavyo na app ya Oky vinafanya kazi vizuri. Tunakusanya hizi taarifa kuwasiliana na wewe juu ya app na huduma zake.



Afya na Hedhi



Taarifa za afya na hedhi yako unazoingiza kwenye kipengele cha kalenda ndani ya Oky app, kama tarehe za hedhi yako ya zamani na hedhi yako ya sasa zinakusanywa na kutumika kutabiri tarehe za mbeleni za hedhi. Taarifa hizi zinatunzwa kwenye servers zetu naunaweza kuzipata pindi uingiapo kwenye akaunti yako kupitia kifaa chochote. Ingawa ili kulinda faragha yako tumeweka mfumo ambao hamna anayewea kumtambua mtumiaji mmoja mmoja kutoka kwenye taarifa zilizohifadhiwa.

Taarifa uingizazo kwenye kadi zako za siku (mwili, unavyojisikia na utokaji wa damu ya hedhi na kadi za dayari yako ya siku) zinahifadhiwa ndani ya kifaa chako na wewe pekee unaweza kuzipata.



Tafiti


Oky kukuuliza mrejesho wako juu ya app ya oky kupitia maswali na tafiti mfano, ufanyaji kazi wa app au utumiaji wa taarifa Oky inazotoa na uzoefu wako kwenye kutumia app ya Oky. Taarifa kutoka kwako kupitia tafiti hizi na maswali zinachukuliwa na Oky kuboresha huduma zetu na uzoefu wako na Oky. Majibu ya tafiti ni ya siri.



Cookies


Cookies ni mafile madogo ya maandishi yanayoitambulisha kompyuta yako, simu, na vifaa vingine kwa server yetu.

Tovuti ya Oky inatumia uchambuzi kutoka Google, ambayo inatumia cookies na teknologia inayofanana kukusanya na kuchambua taarifa juu ya matumizi ya tovuti na kutoa ripoti ya shughuli na yanayovuma. Unaweza kujifunza zaidi juu ya ufanyaji kazi wa Google’ kwa kwenda https://www.google.com/policies/privacy/partners/

Ingawa uchambuzi wa Google unaondoa kila taarifa binafsi juu watumiaji wa tovuti ya Oky(kama anuani ya IP) kabla uchambuzi wowote haujashirikishwa na Oky timu, kwahiyo chambuzi zote za tovuti zinatolewa utambulisho na haziwezi kutumika kukutambua wewe au mtu mwingine.

Tunaweza kukusanya taarifa zilizokusanywa kwa pamoja kupitia app ya Oky kwa uchambuzi wa kitakwimu na matumizi ya kisheria, ikiwemo masoma ya utafiti ili kuboresha uelewa wetu juu ya matumizi ya teknolojia na vifaa vya kidigitali kwa watoto/ vijana wadogo. Matokea ya tafiti hii yanaweza kushirikisha watu wengine kama wadau, wafuasi, waelimishaji na watafiti kupitia mikutano, makala na machapisho. Tukifanya hivi taarifa zote zitakusanywa pamoja na zitakuwa hazina utambulisho

Sheria


Tunaweza kutumia taarifa zako binafsi kutekeleza vigezo vyetu vya matumizi, kutetea haki yetu kisheria, na kufuata jukumu letu kisheria na sera zetu za ndani

2.Tunalindaje taarifa zako

Tunatumia rasilimali nyingi – fidhikali na kieletroniki – kuzuia taarifa zako binafsi dhidi ya kuchukuliwa bila ruhusa na kuwekwa wazi. Ingawa, siku zote kuna uwezekano kwamba watu wa nje wanaweza kinyume na sheria kuingilia au kupata taarifa zako binafsi au mawasiliano yako binafsiIngawa, tunafanya kazi kwa bidii zote kulinda taarifa zako binafsi, hatuwezi kukuhakikishia kwamba taarifa zako au mawasiliano yako yatabaki kuwa ya binafsi .

Taarifa zifuatazo zimehifadhiwa kwenye serverszetu; jina la mtumiaji, mwezi na mwaka wakuzaliwa, jinsia, eneo (inchi na kijiji), taarifa juu ya hedhi yako, tarehe ya kuanza na kumalizika kwa mzunguko wa hedhi na maudhui, lugha na avatar uliyochagua kwenye app ya Oky. Pia tumeweka mfumo ili kwamba mtu yoyote hawezi kutambua mtumiaji kupitia taarifa hizi tulizohifadhi. Tunahifadhi taarifa hizi kwenye server yetu ili uweze kupata taarifa hizi unapoingia kwenye akaunti yako kupitia kifaa tofauti.

Unaweza kuwasiliana nasi juu ya maswali yoyote uliyonayo juu ya ulinzi wa taarifa kupitia mambo@oky.co

3.Maoni juu ya kulinda taarifa zako

Tunaamini tishio kubwa kwenye usalama na faragha ya taarifa zako ni mtu ambaye unamjua—anaweza kutumia kifaa chako. Taarifa unazoingiza Oky ni za faragha na zinatakiwa kubaki kuwa hivyo. Tumeonesha njia ambao unaweza kuweka kifaa chako kiwe salama hapa chini

Anzisha PIN ya kipekee au neno lasiri kuweza kuingia. ifanye iwe ya binafsi na vigumu watu wengine kukisia. usitumie siku yako ya kuzaliwa au jina lako, mfano. kama utatumia kifaa chako na wengine, anzisha PIN ya kipekee au neno la siri kuhakikisha wewe ni mtu pekee unayeweza kupata taarifa za Oky-kwenye kifaa chako . Tengeneza sehemu ambayo itakusaidia kufuta taarifa zako zote kutoka kwenye kifaa chako kama kimepotea au kuibiwa. Kwa Android, pakua na weka tafuta kifaa changu (zamani ni Android Device Manager) kutoka Google Play Store na, kama itahitajika, tumia tovuti interface iliyounganishwa kufunga au kufuta simu yako ukiwa mbali.

4.Tovuti nyingine

App ya Oky au tovuti inawea ikawa na viunganishi vya tovuti nyingine ambavyo havipo chini ya sera faragha hii. Sera faragha hii inahusika tu kwenye uchambuzi wa taarifa zako na Oky. Haishughuliki na hatuwajibiki juu ya faragha, taarifa au matendo mengine ya watu wengine ikiwemo mtu mwingine anayeendesha site au huduma ambayo tovuti ya Oky au app inaunganishwa nayo.

site au huduma na UNICEF. Tafadhali fahamu kwamba vigezo vya sera faragha hii havihusiki kwa tovuti za nje au mada au ukusanyaji wa taarifa zozote pindi utakapo bofya viunganishi vya tovauti za nje.

App ya Oky au tovuti inawea ikawa na viunganishi vya tovuti nyingine ambavyo havipo chini ya sera faragha hii. Sera faragha hii inahusika tu kwenye uchambuzi wa taarifa zako na Oky. Haishughuliki na hatuwajibiki juu ya faragha, taarifa au matendo mengine ya watu wengine ikiwemo mtu mwingine anayeendesha site au huduma ambayo tovuti ya Oky au app inaunganishwa nayo.

site au huduma na UNICEF. Tafadhali fahamu kwamba vigezo vya sera faragha hii havihusiki kwa tovuti za nje au mada au ukusanyaji wa taarifa zozote pindi utakapo bofya viunganishi vya tovauti za nje.

5.Ni kwamuda gani Oky inakaa na taarifa zako

Tutatumia na kutunza taaarifa kwa muda ambao zinahitajika kutumika kwa dhumuni tulilozikusanya na kwa namna inavyoelezewa ndani ya sera ya kushikilia ya UNICEF. Tunatumia taarifa zako kama inavyohitajika ili kufuata jukumu letu la kisheria, kutatua migogoro na kushinikiza makubaliano yetu na haki au kama siyo ya kiteknikali na yenye sababu ya kuziondoa. Pia tunabaki na haki ya kuhifadhi taarifa zako na watu wengine nje ya uthibiti wa moja kwa moja wa UNICEF kama vile; servers na database ya taasisi za watu wengine.

6.Jinsi gani unaweza kudhibiti taarifa zako

Kama umeandikisha akaunti na sisi unaweza kupata taarifa nyingi zinazohusu akaunti yako kwa kuingia ndani na kutumia akaunti settings . Kama unataka kufuta akaunti yako na/au mada ulizochangia unaweza kuzifuta kutoka kwenye app. Pindi utakapofuta akaunti yako taarifa zote zitafutwa kwenye servers zetu

7.Taarifa za mabadiliko kwenye Sera Faragha

Tunapitia mfumo yetu ya ulinzi na sera faragha na tunaweza kurekebisha sera zetu kadri tunavyoona inahitajika. Kama tukifanya mabadiliko kwenye utendaji wetu wa mambo ya faragha, tutaweka taarifa kwenye tovuti ya Oky na kutaarifu kuwa sera faragha imerekebishwa
Mabadiliko haya yataanza moja kwa moja baada tu ya kuziweka kwenye app ya Oky na tovuti. Kwa sababu hii, tunakuhamasisha kuangalia mara kwa mara sera faragha yetu. “tarehe ya iliyoboreshwa ya mwisho” iliyopo chini kwenye ukurasa huu inaonesha ni lini sera faragha ilipitiwa mara ya mwisho
Kuendelea kwako kutumia app ya Oky au tovuti kufatana na mabadiliko haya kunamaanisha umekubali sera faragha iliyopitiwa upya.

8.Wasiliana nasi

Tunapitia mfumo yetu ya ulinzi na sera faragha na tunaweza kurekebisha sera zetu kadri tunavyoona inahitajika. Kama tukifanya mabadiliko kwenye utendaji wetu wa mambo ya faragha, tutaweka taarifa kwenye tovuti ya Oky na kutaarifu kuwa sera faragha imerekebishwa.
Mabadiliko haya yataanza moja kwa moja baada tu ya kuziweka kwenye app ya Oky na tovuti. Kwa sababu hii, tunakuhamasisha kuangalia mara kwa mara sera faragha yetu. “tarehe ya iliyoboreshwa ya mwisho” iliyopo chini kwenye ukurasa huu inaonesha ni lini sera faragha ilipitiwa mara ya mwisho.
Kuendelea kwako kutumia app ya Oky au tovuti kufatana na mabadiliko haya kunamaanisha umekubali sera faragha iliyopitiwa upya.

Ni ya Binti kutoka kwa Binti

Tumia Oky

Wasiliana nasi