mambo@oky.co.tz
1.Makubaliano ya mtumiaji
Hivi vigezo vya matumizi ni makubaliano kati yako na Oky ambayo yanaweka utaratibu wajinsi ya kuitumia app na tovuti ya Oky.
Oky ni kifuatilia hedhi kwa wasichana na kimetengenezwa na wasichana. Inatoa taarifa juu ya hedhi kwa njia ya kufurahisha, yaubunifu na chanya.
Tafadhali soma vigezo vya utumiaji kwa makini. Kwa kutumia app ya Oky, unakubali kwamba umesoma, umeelewa na umekubaliana na vigezo na masharti hapo chini. Kama hukubaliani na kigezo na sharti lolote lile, tafadhali usitumie app ya Oky.
Oky inalenga watoto kuanzia miaka 10 na zaidi. Kama upo chini ya miaka 16 tunakuhamasisha ujadili matumizi na ushiriki wako kwenye app ya Oky na wazazi au walezi wako kuhakikisha wanakubali utumie app ya Oky .
Vigezo hivi vya utumiaji vinaweza kubadilika, tafadhali hakikisha unaangalia vigezo vya matumizi ya app kwenye tovuti mara kwa mara. Tarehe ya mabadiliko ya siku za karibuni itakuwa chini ya ukurasa huu. Ukiendelea kutumia app ya Oky ina maanisha umekubali mabadiliko yoyote au upitiwaji wa hivi vigezo vya matumizi.
Faragha yako ni muhimu sana kwetu– tafadhali soma pia sera yetu ya faragha ambayo itakuonesha jinsi app ya Oky inavyokusanya, hifadhi na kutumia taarifa ulizotupatia. Kwa kutumia app ya Oky unathibitisha kwetu kwamba umekubaliana na sera faragha yetu.
2.Utengenezaji wa akaunti na usalama
Baada yakutengeneza akaunti, utatakiwa uchague swali la siri na utoe jibu. Tafadhali tunza taarifa hizi maana ndiyo njia pekee yakuweza kupata akaunti yako kama ukisahau neon lako la siri.
Baada yakutengeneza akaunti unaweza kurekebisha jina lako unalotumia au linaloonekana kwa kuchagua jina tofauti, badili neno la siri au badili swali la siri na neno la siri.
Kuona jinsi tunatumia taarifa zako binafsi, tafadhali angali sera yetu ya faragha.
Unajukumu la kutunza neno lako la siri, swali lako la siri na jibu la siri na kuilinda akaunti yako. Unajukumu kwa matumizi yote ya akaunti yako, ata kama akaunti yako inatumiwa na mtu mwingine. Huruhusiwi kutumia akaunti ya Oky ya mtu mwingine bila ruhusa yao.
Kama una sababu yoyote yakuamini kwamba akaunti yako haipo salama– kama neno la siri limeibiwa, kwa mfano– utatakiwa kubadilisha neno la siri haraka iwezekanavyo. Kama umesahau neno la siri, utaweka uweke jibu la siri ili iweze kupata akaunti yako.
Kama umesahau swali na jibu lako la siri, utapata nafasi yakujaribu, ila kama utashindwa kukumbuka itakubidi utengeneze akaunti mpya ili uweze kuendelea kutumia app ya Oky. Ukitengeneza akaunti mpya tafadhali kumbuka kwakmba hutaweza kupata taarifa zako za awali zilizokuwa kwenye ile akaunti yako nyingine.
Kama umesahau swali na jibu lako la siri, utapata nafasi yakujaribu, ila kama utashindwa kukumbuka itakubidi utengeneze akaunti mpya ili uweze kuendelea kutumia app ya Oky. Ukitengeneza akaunti mpya tafadhali kumbuka kwakmba hutaweza kupata taarifa zako za awali zilizokuwa kwenye ile akaunti yako nyingine.
3.Mada
Oky ni nia yakufuatilia na kujifunza juu ya mzunguko wako wa hedhi, pia inatoa taarifa juu ya hedhi yako na afya ya mwanamke. Huduma inatolewa bure kwa matumizi binafsi. Kila kitu ndani ya Oky ni kwaajili yako na wenzako ila siyo kwa matumizi ya kibiashara,
Tafadhali usitumie app ya Oky kama njia ya kuzuia mimba au kwa matumizi ya kiafya. Ikitokea tatizo lolote binafsi la kiafya, onana na mtaalamu wa afya.
Oky haikusudii kuchukua nafasi ya vizuizi vya kuzuia mimba na/au kifaa cha afya. Inakusudia kutoa taarifa tu. Kwa kutumia app ya Oky unakubali kuitumia kwa kilichokusudiwa tu na siyo kama njia ya kuzuia mimba au kwa kusudi la mambo ya kiafya.
Ukitoa mada zilizotengenezwa na mtumiaji, Oky inamiliki na kubaki na haki zote ndani ya Oky code, muundo, utendaji na ubunifu wa app ya Oky, na programu, taarifa za msaada au mada zitolewazo kupitia site hii (kwa ujumla “Oky IP”). Ukiacha haki zozote ambazo umeambiwa moja kwa moja umepewa chini ya vigezo vya matumizi, hujapewa haki yoyote ndani ya Oky au haki juu ya Oky. Kama unataka kutumia Oky IP kwa namna ambavyo hairuhusiwi chini ya vigezo vya utumiaji kwanza unatakiwa kuwasiliana na timu ya Oky na kupata ruhusa.
Mpaka isemekane vinginevyo, taarifa zote zitolewazo na Oky kwenye app na tovuti vimesajiliwa chini ya Creative Commons license: Attribution 4.0 International (CC BY 4.0). Leseni hii inaruhusu wewe na wengine kutoa nakala na kusambaza mada kwenye app ya Oky. Leseni hii inakutaka kumtaja mmiliki wa taarifa zote unazotumia. Unapotumia taarifa zozote za Oky, tafadhali tumia viashiria: “Oky imetengenezwa na UNICEF”. Angalia http://www.oky.co.tz. Kama bado una maswali, kwa huru kutembelea the Creative Commons FAQ page, ambapo utapata taarifa zaidi.
Tafadhali kumbuka app ya Oky na taarifa za msaada zinaweza kuwa na picha, sauti na video ambazo zinamilikiwa na watu wengine. Hakuna chochote ndani ya vigeo hivi vya matumizi au Creative Commons license unazuia au kupunguza hati miliki ya watu wengine. Hautatumia taarifa hizi kulebo, kutangaza au kufadhili bidhaa au huduma yoyote. Unajukumu la kipekee kwa uvunjaji wa hati miliki za watu wengine unaosababishwa na utumiaji mbovu wa taarifa hizi.
Majina na nembo za Oky, app ya Oky na UNICEF zinamilikiwa na UNICEF. Zinalindwa chini ya sheria za kimataifa na kitaifa. Matumizi bila ruhusa hayaruhusiwi. Hazitakiwi kutolewa nakala au kutengenezwa tena kwa njia yoyote ile bila ruhusa ya maandishi kutoka UNICEF kwanza. Maombi ya ruhusa yatumwe kwetu kupitia mambo@okyapp.info
4.Vigezo na masharti
UNICEF hurekebisha vigezo hivi mara kwa mara. Kila utumiapo tafadhali angalia hivi vigezo kuhakikisha umeelewa vigozo vinavyotumika kwa muda huo.
5. Viunganishi vya nje na rasilimali
Oky ni app ambayo ipo wazi na inakaribisha watoto wa dunia nzima. Kwasababu ya utofauti wa watumiaji wetu, Oky ina lengo la kutengeneza mazingira ambayo motto yoyote atajisikia huru kusipokujali utaifa, jinsia, tamaduni, dini, mwelekeo wa kijinsia au imani za kisiasa zake .
Maadili ya msingi ya Oky ni kuwa chanya, uwazi, heshima, kujumuisha, maongezi, kushirikiana na kutengeneza .
br>
6.Onyo
Usomacho kwenye app ya Oky au tovuti siyo lazima imeandikwa na timu ya Oky au wafanyakazi wa UNICEF, kwahiyo mawazo na maoni yanayotajwa kwenye app ya Oky na tovuti siyo lazima yawe sawa nay ale ya UNICEF na timu ya Oky.
Mada zote Oky inazotoa au zinatolewa “kama zilivyo” hii inamaanisha hatuwezi kukuhakikishia vyote uvikutavyo kwenye site hii vitakuwa sahihi kabisa au bila kosa. Mada ya Oky inaongezwa kwa kipindi Fulani, inabadilishwa, inaboreshwa bila taarifa ya kabla. Hakikisha unatumia mada kwenye app ya Oky au tovuti kwaumakini na kwakuwajibika.
App ya Oky na tovuti inaweza kuboreshwa na kubadilishwa mar aka mara ili kutoa taarifa zilizoboreshwa, viunganishi au kutoa matumizi mapya na kuangalia mabadiliko ya mahitaji ya watumiaji wetu.
Hatukuhakikishii kwamba app ya Oky au mada zozote ndani yake zitapatikana siku zote au zisikatishwe. Tunaweza kusimamisha au kuondoa au kuzuia upatikanaji wa sehemu yoyote ya app ya Oky kwa uendeshaji au sababu zozote zile. Tutajaribu kukupatia taarifa kabla ya kusimamisha au kuondoa .
Unakubali kwamba unajukumu la kipekee kwa ishu yoyote utakayokutana nayo kutokana na matumizi yako ya app ya Oky. Hakuna namna yoyote UNICEF na/au Oky inawezakuwajibishwa kwa uharibifu au kuumia kunakotokana na utumiaji wako wa app ya Oky.
Unakubali kufidia kwa gharama yako, UNICEF, maafisa, wafanyakazi, washauri na wakala juu ya madai yoyote ikiwemo gharama zako na matumizi ya watu wengine inayotokana na utumiaji wa app ya Oky na tovuti .
Kutajwa kwa majina ya kampuni Fulani au bidhaa kwenye app ya Oky haimaanishi lengo lakuchukua hati miliki, wala isitafsiriwe kama ufadhili au pendekezo kutoka UNICEF na/au Oky.
Matumizi ya baadhi ya sehemu za inchi au maeneo au ramani kwenye site hii hakuashirii nafasi ya UNICEF na/au Oky juu ya hali ya sheria kwenye wa ichi hizi au maeneo, utawala wao na taasisi au uzuiwaji wa mipaka yao.
7.Wasiliana nasi
Kama una swali lolote juu ya Oky, tafadhali wasiliana nasi kupitia mambo@oky.co.tz
8.Sheria za utumiaji
Oky ni app ambayo ipo wazi na inakaribisha watoto wa dunia nzima. Kwasababu ya utofauti wa watumiaji wetu, Oky ina lengo la kutengeneza mazingira ambayo motto yoyote atajisikia huru kusipokujali utaifa, jinsia, tamaduni, dini, mwelekeo wa kijinsia au imani za kisiasa zake
Maadili ya msingi ya Oky ni kuwa chanya, uwazi, heshima, kujumuisha, maongezi, kushirikiana na kutengeneza
Unakubaliana kufuata sheria zote na taratibu ndani ya inchi yako unapotumia app ya Oky